Vyuo Tanzania

Tafuta chuo, kozi, na taarifa kwa urahisi.

Kuhusu Sisi

Karibu kwenye VyuoFinder (University Portal), jukwaa lako namba moja linalokurahisishia kupata taarifa zote unazohitaji kuhusu elimu ya juu nchini Tanzania.

Dira Yetu

Tunaamini kila mwanafunzi ana haki ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati ili kufanya maamuzi sahihi juu ya elimu yake ya baadaye. Dira yetu ni kuwa kitovu kikuu cha taarifa za vyuo vyote (Universities and Colleges) Tanzania.

Tunachofanya

  • Kukusanya na kupanga orodha ya vyuo vilivyopo Tanzania.
  • Kutoa taarifa za kozi (programmes) zinazotolewa na vyuo mbalimbali.
  • Kuonyesha sifa na vigezo vya kujiunga kwa kila ngazi (Certificate, Diploma, Degree, na Masters).
  • Kurahisisha utafutaji ili uweze kuchuja vyuo na kozi kwa urahisi zaidi.

Kwanini Utuchague?

Badala ya kupitia tovuti za vyuo tofauti tofauti kwa wakati mmoja, tumeweka kila kitu sehemu moja kwa muonekano rahisi na wa kisasa unaofanya kazi vizuri kwenye simu yako na kompyuta.